Tuesday 23 February 2016

Barcelona kufungua shule ya soka nchini Nigeria


Gavana wa Lagos Akinwunmi Ambode amearifu kwamba kilabu ya Barcelona inapanga kufungua shule ya soka mjini humo ambayo itakuwa ndio ya kwanza kufunguliwa barani Afrika.
Ambode alitangaza mpango huo baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wakuu wa kilabu yaBarcelona kutoka Uhispania.
Akibainisha umuhimu mkubwa wa michezo katika maendeleo ya bara la Afrika, gavana Ambode alisema kwamba mpango huo utawafungulia njia vijana wenye kipaji cha soka na pia kutoa ajira.
Mmoja wa viongozi wakuu wa Barcelona pia aliarifu kuchagua Nigeria kuwa kama kituo cha ujenzi wa shule ya soka kutokana na idadi kubwa ya watu ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.

No comments: