Thursday 10 March 2016

LIGI KUU TANZANIA NA MATOKEO YAKE

Hatime Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea siku ya Jumatano kwa michezo minne kupigwa.

Mpambano ulikua mkali katika uwanja wa  Mkwakwani mkoani Tanga , Coastal Union waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Jkt.Mpambano.

Huku Tanzania Prison wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Sokoine walitoshana nguvu na Kagera Sugar kwa kufungana bao 1-1.

Kwa upande mwengine Nao Mwadui Fc wakikipiga na Majimaji wametoshana nguvu kwa sululu ya 0-0,JKT Ruvu wakawachapa Toto African kwa mabao 2-0.


Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa Simba kucheza na Ndanda FC,Mbeya City watawaalika Staind United, katika dimba la Sokoine.

No comments: