Thursday 10 March 2016

Livepool na Manchster United kukipiga


Mechi ya siku ya Alkhamis baina  Livepool na Manchster United  katika kombe la Europa  imetajwa kuni ni mechi kubwa zaidi itakayo sisimua mashabiki wengi duniania

Kauli hiyo imetolewa leo hii na Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp. 

Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.

Klopp anasema :”itakua ni ni Mechi kubwa sana.ingawa  haitokua kubwa  zaidi ukilinganisha na kazi yangu  kama mkufunzi watimu ya  Liverpool lakini tutuaishulikia vizuri”

Timu ya Manchester United imeshinda makombe 3 ya bara Europa hivi karibuni ikiwa 2008,huku Liverpool ikilibeba kombe hilo mara tano.


Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.

No comments: