KAMPENI "FICHUA VIPAJI"
Taarifa zinaonesha kuwa watanzania wengi wanasumbuliwa na
maradhi mbalimbali katika miiliyao kama vile pressure, msongo wa mawazo, uzito
mkubwa na mengineyo.
Hali hiyo imedaiwa kua inasaidiwa na mtu kutofanya mazoezi
kwani mazoezi ni moja kati ya kinga ya maradhi mengi na yanapelekea mtu kuwa
sawa kiafya.
Hayo yamebainishwa na mmoja miongoni mwa wachezaji wa mchezo
wa ngumi aina ya Karati (shaurin) nchini Tanzania kutokea Kigogo Mburahati
Uwanja wa Kifa
Balasa Nassor Khalfan alipokua
akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA katika mwendelezo wa kampeni ya “FICHUA
VIPAJI” inayowatafuta wanamichezo mbalimbali kwa lengo kuwaonesha kwa wadau na
kuwainua ili kufikia malengo yao kwa haraka kama walivyojipangia.
Khalfan ni mchezaji mahiri wa mchezo huo na mengi tuliongea
yanayahusu moja kwa moja katika ngazi za michezo na maongezi yetu yalikua kama
yafuatavyo.
Salma: wewe ndio umeshajiingiza huku katika michezo alau unamatumaini
na malengo unawambia nini vijana wenzako?
Khalfan: siku nyingi
huwa nawaambia vijana wenzangu
,jamani tusikae tu nyumbani kufuga miili
tunajenga maradhi tufanye sana
mazoezi kwa ajili
ya afya zetu .
kweli watu nawaambia
sana na
matunda yake yataonekana tu.
Salma: Tanzania kunaonekana kuna michezo mingi lakini ipo
chini tofauti na nchi za wenzetu
zinavyosifika ni upi ushauri wako ili kukuza michezo nchini kwetu?
Khalfan: ushauri
wangu tunaiomba serekali
itutengenezee sehemu maalumu
ya kufanyia michezo
na hasa sisi
watu wa karate, naamini tukipata sehemu nzuri za
kuchezea nchi yetu itasifika tu maana tunaweza.
Salma: una malengo gani katika mchezo wako huu katika siku za usoni?
Khalfan: malengo
yangu ni kufika
mbali zaidi katika
mchezo huu, baadae
niweze kuipeperusha bendera
yangu ya Tanzania
katika mashindano mbalimbali
ndani nje ya
tanzania.
Amemalizia kwa kutoa ushauri kwa serikali kuandaa mbinu maalum
kwaajili ya kuinua viwango wa wanamichezo nchini ili kukuza sekta hiyo huku
akizidi kutilia mkazo kufanya mazoezi kwani kufanya hivyo kutamkinga mtu na
mashambulio ya maradhi mbalimbali yanayomnyemelea.
No comments:
Post a Comment