Siri
imefichuka kwa upande wa timu ya KVZ ambayo inashiriki ligi kuu soka Zanzibar
kanda ya Unguja ambapo Mtandao huu ulitaka kujua ni sababu ipi ilopelekea timu
hiyo kuwa na kasi zaidi kwenye mzunguko huu wa lala salama ambapo wametoka
nafasi ya 12 kwenye mzunguko wa kwanza na sasa wapo nafasi ya 2 kwenye msimamo
wakiwa na alama 29.
Muandishi wa
habari hii amemtafuta Khamis Abdul-hamid Hamid ambae ni katibu mkuu wa timu
hiyo na kutaka kujua nini siri ya mafanikio yao.
Katibu huyo
alisema ujio wa kocha Gwiji katika timu yao Abdul ghani Msoma na kupewa vyeo
wachezaji wao 12 waliopandisha daraja timu hiyo ndizo sababu mbili kuu
zilizopeleka mafanikio na mabadiliko makubwa klabuni kwao.
“ Kwa kweli
siri ya mafanikio yetu ni ujio wa kocha Msoma na pia jeshi la KVZ limewapa
nyota 2 wachezaji 12 waliopandisha timu msimu uliopita, ndo maana unawaona
wachezaji wana ari sana sasa”. Alisema Khamis.
Wachezaji 12
wa KVZ walioengezwa cheo kutoka private mpaka kuwa COPROL ni Salum Songoro, Ali
Mustafa, Suleiman Abdi (Sele Tz), Suleiman Ali, Rashid Maulid na Khatib Khamis.
Wengine ni
Abdallah Suleiman, Abas Abdallah, Nassir Bakar, Makame Ali, Yakoub Bakar na
Mussa Bakar (Edi Enzi).
No comments:
Post a Comment