Sunday 10 April 2016

Bidhaa za spoti za Kobe Bryant kuuzwa kwa bei ya juu zaidi.

Bidhaa za spoti za Kobe Bryant kuuzwa kwa bei ya juu zaidi

Mashabiki wa Kobe Bryant watengezewa bidhaa maalum za spoti kwa ajili ya kumbukumbu ya nyota huyo NBA

Mashabiki wa mpira wa kikapu na wapenzi wa nyota wa L.A Lakers Kobe Bryant, wametengezewa bidhaa maalum za spoti kwa ajili ya kumkumbuka mchezaji huyo baada ya kustaafu.

Bidhaa hizo zilizochapishwa nambari 24 inayoashiria jezi aliyokuwa akivaa Kobe Bryant wakati wa uchezaji wake, zitauzwa kwa bei inayofikia hadi dola 38,000.

Miongoni mwa bidhaa hizo ni kama vile kofia,flana na koti ambayo yataanza kuuzwa rasmi kuanzia wiki ijayo baada ya Kobe Bryant kustaafu rasmi.

Wiki ijayo, Kobe Bryant atachezea L.A Lakers mechi yake ya mwisho ya NBA dhidi ya Utah Jazz katika uwanja wa Staples Center. Bei ya tiketi za mechi hiyo itaanzia dola 670.

No comments: