Sunday 3 April 2016

DOGO MORO JANA WASHINDWA KUFURUKUTA PEMBA


Timu ya Dogo Moro jana imeshindwa kufurukuta mbele ya timu ya Mwenge ya Wete baada ya kupokea kipigo cha magoli 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Pemba uliochezwa jana kwenye uwanja wa Gombani.

Mahudhurio ya mashabiki katika mchezo huo hayakuwa makubwa kama ilivyokuwa juzi katika mchezo baina ya wakongwe Jamhuri na Chipukizi hii ni kutokana na hali ya hewa kuwa ya mawingi tokea jana asubuhi.

Magoli mawili ya Mwenge yaliyofungwa kwa muda mfupi katika dakika ya 16 kupitia Suleiman Abdul-malik na lile lilifungwa na Salum Mussa kwenye dakika ya 17 yalitosha kuwahakikishia kuondoka na ushindi katika mchezo huo.

Hadi Mapumziko Mwenge walikuwa wameshajipatia mabao mawili huku Dogo Moro wakiwa hawajapata kitu.

Goli la tatu la Mwenge liliwekwa tena kimyani na Salum Mussa katika dakika ya 50.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa Dogo Moro liliwekwa wavuni na Mchezaji Ahmed Omar katika dakika ya 80.


Hadi Mwisho wa mchezo huo uliochezeshwa na Suleiman Kisauti akisaidiwa na Suleiman Juma, na Hassan Gerei Mwenge 3 na Dogomoro1.

No comments: