Tuesday 5 April 2016

Kocha Conte kutua Chelsea msimu ujao


Chelsea yatangaza kutia saini mkataba na kocha mpya Antonio Conte


Kilabu ya Chelsea nchini Uingereza imemtangaza rasmi Antonio Conte kuwa kocha wake mpya atakayekinoa kikosi chake kuanzia msimu ujao.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa mtandaoni leo hii kupitia tovuti rasmi ya Chelsea, Conte alitia saini mkataba wa miaka 3.
Chelsea iliamua kuchukuwa uamuzi huo kutokana na matokeo duni yasiyoridhisha tangu mwanzoni mwa msimu huu.
Conte ambaye kwa sasa anaendelea kufunza timu ya taifa ya Italia, anatarajiwa kuondoka baada ya mashindano ya EURO 2016.

No comments: