Sunday 10 April 2016

Real Madrid yapooza maumivu ya UEFA kwenye ligi ya La Liga.



Real Madrid yaicharaza Eibar bao 4 kwa nunge kwenye uga wa Santiago Bernabeu.
Real Madrid yapooza maumivu ya UEFA kwenye ligi ya La Liga

Timu ya Real Madrid iliikaribisha Eibar nyumbani Santiago Bernabeu kupambana nayo kwenye mechi ya ligi kuu ya soka ya La Liga nchini Uhispania.

Real Madrid ilianza kwa kishindo mwechi hiyo na kutangulia kufunga bao 4 katika kipindi cha kwanza ili kujihakikishia ushindi wa mapema.

Magoli ya Real Madrid yalifungwa na James Rodriguez, Lucas Vazquez, Cristiano Ronaldo na Jese Rodriguez.

Wachezaji wa Eibar ambao walikuwa na wakati mgumu katika mechi hiyo, walishindwa kupenyeza kwenye ngome ya ulinzi ya Real Madrid na kuambulia patupu bila ya kupata goli la kufutia machozi.

Ushindi huo wa 4-0 dhidi ya Eibar umeiwezesha Real Madrid kukusanya jumla ya pointi 72 baada ya wiki 32 za ligi ya La Liga.

No comments: