Thursday 7 April 2016

TAIFA WALA SAHANI MOJA NA CHWAKA.




Hatua ya sita bora ya ligi daraja la kwanza taifa kanda ya Unguja leo imeendelea tena katika uwanja wa Amani kwa kuchezwa mchezo kati ya timu ya Wakombozi wa ng’ambo Taifa ya Jang’ombe  walipopepetana na Chwaka.

Katika mtanange huo Taifa ya Jang’ombe wamekula sahani moja na Chwaka baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Mchezo huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani, Chwaka walikuwa ndio wa mwanzo kuliona lango la Taifa kupitia mchezaji Kassim Khamis katika dakika ya 19.

Mtanange huo ulikuwa wa kasi kwa kufanya mashambulizi kwa kila upande na ndipo mchezaji wa Taifa  Yussuf Mariano aliposawazisha katika dakika ya 44, na timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.

Na mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.

Matokeo hayo yameifanya timu ya Taifa ya Jang’ombe kuwa nafasi ya kwanza na  alama nne (4) ambazo sawasawa na timu ya Mundu, na Chwaka wao wapo nafasi ya tatu (3) na alama mbili (2).

Katika michezo waliyokutana timu hizo katika mzunguko wa kwanza na wa pili Chwaka walipoteza mechi zake zote dhidi ya Taifa, hivyo leo imeonekana kuondoa uteja wao kwa kuwabana Taifa kwa kutoka sare ya bao 1-1.

No comments: