Sunday 10 April 2016

VIJANA WAZIDI KUTOANA JASHO PEMBA


KAMPENI "FICHUA VIPAJI"


Michuano ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 Wilaya ya Chake Chake imerindima jana na leo katika uwanja wa Gombani ikiwa ni hatua ya Nane Bora.

Jana Jumamosi kulikuwa na michezo miwili, saa mbili asubuhi ikiwa ni kati ya Ajax na Small Younng Islanders na saa 4 kukifanyika mchezo baina ya Real Mkoroshoni na Stone City.

Katika mchezo wa asubuhi timu ya Ajax imefanikiwa kuibuka washindi kwa magoli 2-1.

S/Y/Islanders ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao lilifungwa na mchezaji wake Khalfan Said katika dakika ya 12.

Bao hilo lilisawazishwa na Ajax kwenye dakika ya 21 kupitia mchezaji wake Abuubakar Habibu huku la pili likiwekwa nyavuni na Said Mbarak Mkude katika dakika ya 44.

Katika mchezo uliochezwa saa 4 asubuhi wa mashindano hayo Real Mkoroshoni wakafakiwa kuondoka na ushindi kama huo wa mabao 2-1.

Goli la Stone City likifungwa na Said Khalfan kwenye dakika ya 28 huku yale ya Real Mkoroshoni yakiwekwa wavuni na Jamal Amir dakika ya 51 na Shakir Aboud Said dakika ya 87.

Michezo ya leo ilikuwa ni kati ya Korea Star Soka na Madungu City saa 2 asubuhi na saa 4 kulikuwa na mchezo kati ya Future Boys na Mabaoni City.

Mchezo wa asubuhi timu za Korea Star Soccer na Madungu City ziliumaliza mchezo huo kukiwa hakuna mbabe kwa kutoka suluhu 0-0.

Ama kwaa mchezo wa saa 4 asubuhi timu ya mabaoni City wameibuka washindiki kwa kuichapa Future Boys kwa bao 1-0.


Ligi hiyo itaendelea tena Jumamosi na Jumapili kwenye uwanja wa Gombani.

No comments: