Friday 8 April 2016

YANGA KUKAMILISHA KAMBI YAKE KISIWANI PEMBA LEO.



Kikosi cha timu ya Yanga ya Dar-es Salaam ambacho kipo kisiwani Pemba kwa kambi maalum ya kujiandaa na mchezo wao na Al-Ahly ya Misri katika michuano ya Klabu Bingwa Africa hatua ya 16 bora asubuhi kinakamilisha mazoezi yake kisiwani humo.

Yanga iliyowasili kisiwani Pemba kwa ajili ya Kambi hiyo Jumatatu imekuwa ikijifua katika fukwe za Wesha kuongeza stamina na uwanja wa Gombani kwa ajili ya kucheza mpira na kuongeza mbinu zaidi.

Baada ya kukamilika mazoezi ya leo asubuhi jioni Yanga watasafiri kurudi jijini Dar es salaam  ambapo kesho watacheza mchezo wao wa kwanza na Al-Ahly kabla ya kurejea tena tarehe 19 mwezi huu huko Misri.

Katika kambi hii ni mchezaji Matheo Antony pekee ambaye jana hakushiriki mazoezi na wenzake na amekuwa alioneka akifanya mazoezi ya kukimbia kutokana na kuwa majeruhi lakini wachezaji wote waliokuja nao hapa Pemba wanaendelea na mazoezi.


Yanga ni mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Klabu Bingwa Africa na ameingia katika hatua hiyo baada ya kuitoa timu ya APR ya Rwanda na akivuuka hatua hiyo ataingia kwenye hatua ya robo fainali.

No comments: