Friday 13 May 2016

JUVENTUS YAREFUSHA MIKATABA YA VIGOGO WAKE WAWILI


Buffon na Barzagli waongezewa mikataba yao na Juventus kwa miaka 2 zaidi

Mabingwa wa Serie A nchini Italia Juventus, wamerefusha mikataba ya wachezaji wao wakongwe wawili kwa miaka 2 zaidi.


Hafla maalum iliandaliwa katika taasisi ya michezo ya Juventus iliyoko mjini Torino ambapo kipa Gianluigi Buffon na Andrea Barzagli walitia saini mkataba hadi mwaka 2018.


Kipa Buffon mwenye umri wa miaka 38 na ambaye amechangia pakubwa mafanikio ya mabingwa hao Italia, ataendelea kulinda lango la Juventus hadi kufikia umri wa miaka 40 kufuatia mkataba huo.

Buffon pia ameweza kuweka rekodi mpya msimu huu kwa kuwa kipa aliyefungwa magoli machache zaidi kwenye ligi.

No comments: