Sunday 15 May 2016

KIJICHI WAENDELEA KUSUASUA LIGI KUU ZANZIBAR

Timu ya kijichi bado imeendelea kufanya vibaya katika mechi zake za ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Wanajeshi wa Kipanga.


Mtanange huo uliosukumwa majira ya saa nane za mchana ndani ya dimba la Amani mjini Unguja,Kipanga walianza kufunga bao la mapema lililofungwa na Nassor Saleh katika dakika ya sita 6, Nassor akarudi tena wavuni kwa kufunga bao la pili mnamo dakika ya 31.

Ndani ya kipindi cha pili katika dakika ya 67 Imran Abdul Rai akaipatia Kipanga bao la tatu 3, na mpira ilimalizika kwa Kijichi kubamizwa kichapo cha mabao 3-0, kutoka kwa Wanajeshi hao wa Kipanga.

Kijichi ni mechi yao ya 21, wakiwa wameshinda michezo miwili, sare michezo tisa 9, na wamepoteza michezo kumi 10, wanashika nafasi ya 12, na alama 15.

Kwa upande wa Kipanga wao pia ni mchezo wa 21, wameshinda mechi saba 7, wamepoteza michezo mitano, na sare michezo tisa 9, wanakamata nafasi ya saba 7, na wana alama 30

 

No comments: