Sunday 15 May 2016

MAFUNZO YATOA KICHAPO CHA MABAO 3-1, KWA BOY’S.


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya Mafunzo imewapa kichapo timu ya Jang’ombe boy’s cha mabao 3-1,katika mchezo wa ligi kuu uliosukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.


Katika mchezo huo uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni, Mafunzo walianza kushinda bao la kwanza lililofungwa na Hassan Ahmad dakika ya 29, dakika chache tu baadae Sadik Habib akaipatia Mafunzo bao la pili alilofunga katika dakika ya 34.

Ilipofika dakika ya 41 mchezaji wa Jang’ombe boy’s, Hafidh Bariki akaachia shuti kali lililomshinda mlinga mlango wa Mafunzo Abdul-swamad Suleiman,  mpira huo uliingia wavuni na kuipatia jang’ombe bao la kwanza.

Mafunzo walijipatia bao la tatu katika dakika ya 65 lililofungwa na Shaban Ali, na mchezo huo kumalizika kwa Mafunzo kuibuka na ushindi mnene wa mabao 3-1.

 Mafunzo sasa wamepanda hadi nafasi  ya pili wakiwa na alama 38, na Jang’ombe boys wapo nafasi ya kumi 10 na wana alama 25.

No comments: