Saturday 14 May 2016

POLISI WAONDOKA NA FURAHA UWANJA WA AMANI.


Timu ya Polisi imeondoka na furaha ndani ya dimba la Amani kufuatia ushindi walioupata, katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa nane za mchana.
Polisi imejinyakulia alama tatu katika mechi hiyo baada ya kuwafunga timu ya Miembeni bao 1-0, lililowekwa wavuni na mchezai Abdallah Omar ndani ya kipindi cha kwanza cha mtanange huo.

Ushindi huo wa Polisi ni wa pili tangu kuanza kwa ligi kuu ya Zanzibar ambapo leo wamecheza mchezo wao wa 21, wamepoteza michezo 11, na sare michezo nane 8, na sasa wamefikisha alama 14, wakiwa nafasi ya 13.

Kwa upande wa Miembeni wao pia wamecheza michezo 21, wameshinda mechi  nane 8, wamepoteza mechi nane 8 na wametoka sare michezo mitano 5. Miembeni wanashika nafasi ya saba 7, na wana alama 30.

 

No comments: