Mchezaji wa timu ya Flammingo Academy ya Dar es salam FADHILI ABDALAY amesme ni vyema kukawekwa vituo maalum kwa watoto vya kukuza viwango walivyonavyo akisema hali hiyo itaweza kukuza utaalamu wao na baadae kukua kwa ajira ya kujiajiri wenyewe.
Ameyasema hayo leo alikua akizungumza na mwanaripota wako kutoka SALMA SPORTS MEDIA walipotembelewa ili kujua changamoto na faida zinazopatikana katika timu yao hiyo.
Amesema wanacheza mpira vizuri na timu yao inafanya vizuri katika mashindani mengi tu lakini kuna uhaba wa wafadhili na wadau wa soka katika ngazi za chini "kama wapo wakubwa na mabosi waje watuone tunacheza vizuri watusaidie"alisema Fadhil
FADHILI ABDALAY ana umri wa miaka 11 nafasi yake uwanjani namba 10 .Timu ya Flammingo Academy ipo katika kiwango cha Junior.
No comments:
Post a Comment