Tuesday, 23 February 2016

KOCHA TOTO AFRICANS: TUNATAKIWA KUFUNGA MAGOLI ZAIDI ILI TUWE SALAMA


Ikiwa wamebakiwa na michezo kumi ya ligi kuu Tanzania Bara (VPL) msimu huu timu ya Toto Africans ya Mwanza imekata tamaa ya kumaliza katika nafasi tano za juu na badala yake kocha mkuu wa timu hiyo, Mjerumani, Dominic amewata wachezaji wake kuhakikisha wanamaliza ndani ya TOP 10.
Toto ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Kagera Sugar ya Kagera katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wikendi iliyopita na kuwafanya wafikishe pointi 22 na kubaki katikati ya msimamo baada ya kucheza michezo 20.
“Kumaliza ndani ya tano bora msimu huu haitawezekana, labda msimu ujao. Lakini endapo tutamaliza nafasi ya nane au ya kumi haitakuwa mbaya”, anasema Mjerumani huyo ambaye timu yake imeshinda mechi tano, sare saba na kupoteza mara nane katika michezo 20.
Toto imekusanya wachezaji wengi vijana ambao hawana uzoefu mkubwa katika ligi” Sisi ni timu changa, wachezaji wetu wengi wanacheza ligi kuu kwa mara kwanza, msimu ujao utakuwa mzuri zaidi”.
Toto imekuwa ikifunga magoli machache katika mechi na hadi sasa wamefanikiwa kufunga jumlaya magoli 19 tu na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 27.
“Lazima tufunge angalu magoli mawili katika mechi ili tuwe salama”, anaongeza kusema Dominic ambaye timu yake ipo nafasi ya tisa lakini kuna tofauti ya pointi saba tu kati yao na timu ya JKT Ruvu inayoburuza mkia.
“Tumekuwa tukishinda, kisha tunapoteza, tunashinda, tunapoteza. Kuna tofauti kubwa unapocheza katika uwanja wa nyumbani na ugenini, kwani unaposafiri safari ndefu mazingira siyo mazuri kwa wachezaji wetu kwa sababu hatuna malazi ya kuridhisha ugenini.”
shaffih dauda.

No comments: