Magoli mawili ya dakiza za 26′ na 49′ yaliyofungwa na mchezaji Hassan Kabunda yameipa timu ya Mwadui FC ushindi wa kwanza katika michezo minne iliyopita ya ligi kuu.
Ushindi huo (nyumbani Mwadui Complex) dhidi ya Coastal Union ya Tanga umeipandisha hadi nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu timu hiyo ya Shinyanga wakiwa na alama 32 pointi moja nyuma ya Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya nne ikiwa na pointi 33.
“Mchezo ulikuwa mzuri, lakini nilichofurahi ni kwamba vijana wangu wamecheza katika maelekezo niliyowatuma ndiyo maana tumeweza kupata ushindi”, anasema kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ambaye timu yake ilipoteza dhidi ya African Sports, Azam FC (ugenini) na kulazishwa sare na Tanzania Prisons (nyumbani.)
“Coastal wamecheza vizuri, si timu mbaya, ikumbukwe wametoka kuzifunga timu mbili za juu katika msimamo (Yanga SC na Azam FC) hivyo ni timu nzuri ambayo imejipanga, tusingekuwa makini tungeweza kupoteza mechi. Nashukuru tumepata pointi tatu muhimu ambazo zina tusogeza juu katika msimamo. Raundi ya pili, ligi imekuwa ngumu sana”, anamaliza kusema kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya bara na ile ya vijana U23 ya Tanzania.
Coasta iliifunga Azam FC kwa bao 1-0 kabla ya kuwavaa Mwadui, bado wameendelea kubaki katika eneo hatarishi la kushuka daraja.
“Sisi tumekubali matokeo. Wala sisi hatuzungumzii maamuzi ya waamuzi, tumecheza mpira, tumefungwa”, alisema kwa ufupi kocha wa Coastal, Ally Jangalu.
shaffih dauda.
No comments:
Post a Comment