Pambano la ligi daraja la kwanza taifa Pemba kati ya timu ya
Mkungu Malofa na Convol lililotarajiwa kupigwa jana 25 Feb. 2016 kwenye uwanja
wa Gombani lilishindwa kufanyika baada ya timu zote kufika kiwanjani zikiwa na
jezi zilizofana.
Timu hizo zote mbili zilidai kuhudhuria katika mkutano wa
matayarisho ya mechi (Pre- match meetng) zilifika kiwanjani hapo zikiwa
zimetinga jezi za rangi ya njano.
Mashabiki kadhaa walikuwa wameshafika na uwanjani kushughudia
mchezo huo ambao ulitarajiwa uwe wa ushindani mkubwa hasa kutokana na nafasi za
timu hizo katika msimamo wa ligi daraja hilo kwa mkoa wa kusini Pemba.
Baada ya kujitokeza hali hiyo wasimamizi wa mchezxo akiwemo
Kamisaa Ali Juma Salim na Mwamuzi Said Ali walizungumza na
viongozi wa vilabu hivyo ili kujaribu kutafuta njia ya kuchezwa kwa mchezo huo
ikiwemo kuzishauri timu hizo kuangalia uwezekano wa kupata jezi nyengine.
Hata hivyo timu ya Convol waliamua kuvaa jezi nyekundu ambazo
walikuwa nazo kama akiba hata hivyo wakatikiwa kubalidisha na kaptura ila
walikuwa hawana nyengine zaidi ya hizo za njano.
Kutokana na hali hiyo mwamuzi alitoa muda kwa timu hizo
kuweza kutafuta jezi ili mchezo huo uchezwe lakini hata hivyo hakuna timu
iliyoweza kufanya hivyo wakidai kila moja ilihudhuria katika kikao na kuonyesha
jezi ambazo watavaa.
Kwa upande wa kocha wa timu ya Convol Kassim Moh`d alisema
kuwa timu yake ilifika katika pre-match meeting na kuanisha jezi ambazo
wengevaa kwa hiyo juhudi waliyoifanya ni kubadilisha fulana za juu ambao ndio
uliokuwa uwezo wao.
Hata hivyo Kocha msaidizi wa timu ya Mkungu Malofa Moh`d
Khamis Othman alisema hakukuwa na haja kwa timu yake kutafuta jezi nyengine
wakati wao walikuwa ndio wageni,pia walifika mapema katika Pre-Match meeting.
Timu ya M/Malofa ambayo ina alama 23 na kushika nafasi ya
pili ilihitaji kushinda mchezo ili kujiimarisha kwenye nafasi hiyo, huku kwa
upande wa wapinzani wao Convol walio na alama 19 na nafasi ya nne walihitaji
kushinda kufikisha alama 22 na kujenmga matumaini ya kuingia katika timu tatu
za juu.
No comments:
Post a Comment