Mchezaji nyota wa timu ya Shein Rangers inayoshiriki ligi daraja la tatu kanda ya Kinondoni Dar es salaam Yasin Witto amesema kua soka la Tanzania lipo chini ya kiwango ukilinganisha na baadhi ya nchi za nje ya Tanzania.
Witto ametoa kauli hiyo alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya hali halisi ya maendeleo ya soka nchini.
Amesema soka la Tanzania halikuwi kutokana na kutokuwepo juhudi za makusudi za kulisukuma soka kwa kuandaa mbinu mbalimbali zenye kusukuma mbele maendeleo hayo.
Amesema mataifa mengine hua wanaweka msingi bora ya soka tangu chini (academy) hatimae kuzaa vipaji bora na kuwa na wachezaji wenye kusifika ndani na nje ya nchi yao lakini hali ni tofauti na nchini Tanzania.
Mbali na academy za watoto alizozisema lakini pia amesema soka la vijana nchini Tanzania halipewei kipao mbele wakati ndani ya vijana haohao ndio kuna wachezaji wazuri na wanaoweza kuliwakilisha taifa.
Amemalizia kwa kutoa wito kwa chama cha soka nchini (TFF) kuangalia zaidi msingi wa soka yaani kwa watoto kwani wakiweza kuwalea vizuri baadae nchini itang’ara kwa wachezaji wazuri na mwishowe soka litakua.
“ningependa chama cha soka nchini kingetoa tamko kama kila tmu iwe na academy na kuwezeshwa kumiliki viwanja vyake wenyewe naamini,hapo soka litakua pia kuwe na mashindano meng ya vjana ukiachana na Airlel na Copa Cocacola yawepo na mengne”alisema Witto.
Witto ni mchezaji hatari katika timu hiyo (jezi nambari 15) anacheza nambari mbili na wakati mwengineu midfield ana umri wa miaka kumi na sita (16) na sifa yake kuu ni kupiga vichwa na kukaba ipasavyo katika eneo lake.
No comments:
Post a Comment