Katika mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya Mjini
uliosukumwa jana ndani ya dimba la Amani mjini Zanzibar, timu ya West coast
imekubali kichapo cha bao 1-0 walipofungwa na Amani Fresh.
Mtanange huo uliosukumwa majira ya saa nane za mchana, timu zote
zilifanya mashanbulizi ya mara kwa mara, pia zilipata nafasi za kushinda lakini
nafasi hizo hawakuzitumia vyema.
Bao pekee la Amani Fresh limewekwa kimyani na mchezaji Rashid
Suleiman katika dakika ya 50 ya mchezo huo.
Baada mchezo huo SALMA SPORT MEDIA ilizungumza na kocha wa
timu ya West coast Issa Ramadhan ili kutaka kufaham kipi kilichopelekea timu
yake kufungwa katika mchezo huo, Kocha Issa amesema walipata nafasi lakini
wameshindwa kuzitumia.
“Tumepata nafasi lakini tumeshindwa kuzitumia na wenzetu wamezitumia
ilo limekuwa tatizo la kila siku, ni umakini tu kwa sababu kila siku
tunafahamishana icho kitu lakini cjui tufanye kitu gani zaid ili wapate
kutufaham, nafikiri ni kufanya mazoezi ya kufunga zaidi tutaendelea kufanya
labda nafikiri wanaweza wakabadilika tunategemea hivyo”. Alisema Kocha Issa.
Vile vile kocha wa timu ya Amani Fresh Said Hakiim Suleiman
amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri kwa timu zote lakini Allah amewaajalia
kushinda wao katika mchezo huo.
“Mchezo ulikuwa ni mzuri na wa nguvu wachezaji wamejitahidi
wa pande zote mbili ispokuwa Allah ametujaalia sisi kushinda, tutatakaa pamoja
ili kuyashughulikia makosa mazoezini, tumebakisha game mbili na kwa uwezo wa
Allah tutaingia katika ya nane 8 bora”. Alisema kocha Said.
Katika mtanange huo timu ya Amani Fresh wamevaa jezi rangi ya kijani na
West coast wamevaa jezi rangi ya blue.
No comments:
Post a Comment