Licha ya kusimama kwa mashindano ya mpira wa Basketball
nchini Zanzibar lakini timu hizo bado
zinaonekana kutovunjika moyo kuendelea kuafanya mazoezi katika viwanja vyake.
SALMA SPORT’S MEDIA katika harakati zake iliwaona wachezaji wa timu ya
New West katika uwanja wa Basketball wa MnaziMmoja mjini Unguja wakiwa wanafanya
mazoezi uwanjani hapo.
Katika harakati hizo SALMA SPORT’S MEDIA ilibahatika kuzungumza
na kocha wa timu hiyo Nassor Salum ili kutaka kujua ni kwa nini wanafanya
mazoezi bila ya kuwepo kwa mashindano yoyote yale kwa sasa na wachezaji
wanaichukuliaje hali hiyo?
Kocha Nassor alisema
kuwa wanafanya mazoezi hayo kutokana na system za chama huwa zinafanya ligi za kushtukiza hivyo inawalazimu kufanya
mazoezi kila mara ili yanapotokea mashindano basi iwe moja kwamoja kushiriki tu
bila ya wasiwasi wowote.
“Tunafanya mazoezi kwa sababu ya kujiandaa sisi kama timu,
huwa tunauzoefu na system ya chama cha Basketball Zanzibar kwa maana kwamba
mara nyingi huwa kinatushtukiza tu ligi zao hazina muda maalum, hivyo sisi kama
New West ni lazima tuwe tunafanya mazoezi binafsi ili hata ikitokea ligi basi
tuwe vizuri”. Alisema kocha Nassor.
Aidha amesema kuwa timu kama timu wanaathirika kutokana na
kutokuwepo kwa ligi yoyote.
“Tunaathirika kwa sababu timu kama timu inapokuwa inafanya
mazoezi kwa muda mrefu wachezaji wanafikia hatua wanachoka, kwa hiyo mtu
anapochoka na hapa hatulipani mwisho mtu anaona abakie nyumbani au afanye shughuli zake nyengine kwa sababu anafanya mazoezi muda mrefu lakini ligi hakuna”.
alisema Nassor
Hivyo ametoa wito kwa Wizara husika na kusema kuwa iache kutazama mchezo mmoja tu
kwani michezo ipo mingi nchini na yote inanafasi nzuri ya kuitambulisha
nchi,hivyo iitazame kama wanavyotazama sasa mchezo mmoja wa mpira wa miguu.
“Wizara iache kujiwekeza katika mchezo mmoja tu na waangalie
na michezo mengine, kwa mfano football toka tunafumbua macho sisi, football
wameing’ang’ania lakini michezo mengine hawakuipa nafasi kiasi ya kwamba hata
football nao hawana wafikapo, lakini wangejaribu siku moja ama miaka fulani
kuangalia hii michezo mengine huenda wakatoa wachezaji wazuri, huenda tukawa
tuna ligi nzuri na pia huenda watu wakatengeza masoko ya uuzaji kwa sababu
Zanzibar Basketball wanaipenda na hiyo football watu wanaipenda lakini kuna
michezo mingi kama Netball, Vollball inakufa kwa sababu haina mashindikizo ya
Serikali”.
Sambamba na hayo pia ameitaka kamati ya Basketball wawe
wabunifu zaidi katika mchezo huo.
“Kamati ya Basketball kama
ipo na inanisikia wawe wabunifu kwa sababu bila ya wao hakuna kitu
ambacho kitafanyika ni lazima wajikubalishe wakae na vilabu wapange”.alimalizia
kusema kocha Nassor.
No comments:
Post a Comment