"KAMPENI YA FICHUA VIPAJI"
Imesemwa kua soka la Tanzania ni lenye kukabiliwa na
changamoto nyingi ambazo kwa namna moja ama nyengineyo hurudisha nyuma malengo
ya wachezaji wa timu nyingi nchini hasa timu ndogondogo.
Kauli hiyo imetolewa leo hii na kocha wa timu ya Vijana Renjers wakati Tonge Nyama Dos Santos alipokua
akizunguza na SALMA SPORT’S MEDIA leo hii katika kampeni ya “FICHUA VIPAJI”
ikiwa ni mchakato wa kuwatembelea, kuwakagua na kuwaonesha hadharani wachezaji
wadogowadogo wenye malengo makubwa na mazuri katika soka.
Amsema wachezaji wamekua wakifanya vizuri sana lakini
changamoto nyingi ndio tatizo.
Akielezea miongoni mwa changamoto hizo ni kama timu kutokua na vifaa vya mazoezi vya kutosha hali inayowafanya wachezaji
kucheza katika mazingira magumu.
Pia maesema hata miundombinu ya viwanja wanavyochezea ni
mibovu hivyo wachezaji hao hucheza tu haliya kua ni tofauti na mchezaji
anavyotakiwa kucheza.
Amemtolea mfano mchezaji KANIY FUNDI wa timu yake akisema, ni
mchezaji mwenye malengo ya juu katika soka, siku moja anatamani awe mchezaji
mwenye kusifika nchini , mchezaji huyu ni fundi wa soka na hata wamashabiki
wengi wanajikuta kumpenda kutokana na kiwangoi chake lakini bado pia yupo
katika mazingira hayo.
Amesema KANIY ni mchezaji mwenye umri wa miaka 20 na anacheza
nambari 9 katika timu hiyo ya Vijana Renjers ana dribo vizuri mpira anapungunguza presha ya mashambulizi pia
anajua kufunga kitaalmu zaidi.
Tonge Nyama Dos Santos ametoa wito kwa wadau wa soka nchini
kuweka mazingira bora ya soka ili wachezaji wacheze katika mazingira mazuri ili
vipaji viibuke.
No comments:
Post a Comment