Monday 7 March 2016

HATA KABLA YA GOLI LAKE DHIDI YA AZAM TAYARI JUMA ABDUL AMETHIBITISHA YEYE NI BORA

Mlinzi wa kulia wa Yanga SC, Juma Abdul, siku ya Jumamosi iliyopita alifunga goli la kusawazisha wakati timu yake ilipokuwa nyuma kwa goli 1-0 dhiya Azam FC. Juma alifunga kwa kiki kali ya mbali na bao lake hilo limekuja baada ya kiwango cha juu kwa muda wa mwaka mmoja sasa.
Akiwa amechangia magoli mengi ya timu yake akicheza kama mlinzi wa kupanda na kushuka katika fullback namba 2, Juma ni kati ya wachezaji ambao wanastahili kupewa mkataba mpya wenye maslai zaidi kwenye klabu ya Yanga ama nje ya timu hiyo.
Mlinzi huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, alijiunga na Yanga, Julai, 2012 akitokea Mtibwa Sugar na hadi sasa tayari ameshinda mataji mawili ya VPL na moja la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati ( Kagame Cup)
2012-2014
Hadi anamaliza mkataba wake wa awali wa miaka miwili klabuni Yanga, Juma hakuwa mchezaji staa lakini kocha Ernie Brandts aliendelea kumjenga mchezaji huyo licha ya kuwa chaguo la pili nyuma ya Mnyarwanda, Mbuyu Twite. Juma alitumia vizuri kila nafasi iliyokuja mbele yake.
Mara kadhaa nilimsisitiza kutokubali kupoteza ari yake, nilicheza na Juma katika timu ya vijana ya Kingalu Kids pale Morogoro, siku zote alitaka kuwa mchezaji bora, ni mtu anayejituma sana, ana nidhamu, msikivu, mvumilivu.
Katika msimu wake wa pili, kuna wakati nilimwambia ‘anakaribia kuwa beki 2 bora Tanzania’ licha ya kwamba hakuwa mchezaji anayetazamwa sana na mashabiki.
Alifikia uamuzi wa kuondoka klabuni hapo kama tu asingepewa mkataba wenye maslai ya juu. Mkataba wake wa kwanza Yanga haukuwa na maslai ya juu sana lakini kutokana na umri wake wa wastani nakumbuka nilimwambia Juma asiondoke Yanga na badala yake azungumze nao vizuri kisha asaini mkataba mpya bila kutazama maslai kwanza.
Juma hakuwa mchezaji wa timu ya Taifa (taifa stars) na wala hakuwa mchezaji mwenye uhakika sana katika kikosi cha kwanza cha Yanga, na kwa mchezaji kijana mara zote hapaswi kushindwa Yanga kwa sababu za kimaslai. Juma alisaini tena mkataba wa miaka miwili kuendelea kubaki Yanga.
2015-16
Amejitolea kwa nguvu zake zote, uwezo wake wote, jitihada zote na sasa kikosi cha Hans Van der Pluijm kinaweza kucheza bila uwepo wake, lakini si kwa tabia ya mashambulizi inayotumika kuanzia Januari, 2015 baada ya Hans kuchukua nafasi ya Mbrazil, Marcio Maximo mwishoni mwa mwezi Disemba, 2015.
Mkataba wa Juma na Yanga unakwenda kumalizika baada ya kumalizika kwa msimu. Nadhani Yanga wanapaswa kufanya haraka kumsaini tena mchezaji huyo na si kufikiria kuwasaini wachezaji wapya. Wanapaswa kumuuliza Hans kama ataendelea kumuhitaji Juma.
Hata kabla ya goli lake dhidi ya Azam FC tayari Juma amejithibisha yeye ni 
(SHAFFIH DAUDA)

No comments: