Saturday, 12 March 2016

MAFUNZO NA KIPANGA HAKUNA MBABE.


Timu ya Mafunzo pamoja na wanajeshi wa Kipanga leo wameshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni.

Mtanange huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa visiswani Zanzibar, timu zote zilicheza mpira wa kushambulia, na hadi mtanage huo unamalizika hakuna mbabe katika mchezo huo.
Akizungumza na SALMA SPORT'S MEDIA, kocha msaidizi wa timu ya  Mafunzo Abdallah Bakar Eddo amesema mechi ni nzuri kimuonekano wa kawaida  lakini ni mbaya kwao ukizingatia kuwa  walitarajia kuibuka na usindi katika mechi hiyo,
"mechi ni nzuri lakini kiupande wetu ni mbaya kwa sababu leo ilikuwa ni mechi muhimu kiupande wetu ili tuweze kushinda ila wachezaji wameshindwa kupokea maelezo kwa sababu tumewapa majukumu wameshindwa kuyafanyia kazi bado tunakazi nyengine ya kuweza kufanya kazi zaidi” alisema kocha Eddo.
“kiujumla leo hawajafanya kazi nzuri katika  uwanja majukumu yote wamefeli hawakuyafanyia kazi lakini wangeyafanyia kazi tungeibuka na ushindi” Aliongeza Eddo.
Kwa upande wa mwenyekiti wa Kipanga Meja Shamhuna amesema kua, mchezo umekwisha salama na wanashkuru, kwani kila mmoja alicheza kwa lengo la kushinda,”
“nia yetu ilikuwa ni kushinda lakini mchezo umekwisha na hatimae tumetoka droo, tumegawana point mojamoja kwa sababu mpira una matokeo matatu kushinda kufungwa na kudroo,kwa hivyo tumegawana point sio mbaya tunaangalia mbele sasa”
Aidha alisema "timu zote zilikuwa zina point 22 na kila mmoja amekuja kwa lengo moja la kutaka kushinda  ndio maana mpira ukawa mgumu kwani kila mmoja alikuwa anataka kushinda mechi ilikuwa taff sana tunashambuliana zamu kwa zamu”
Mafunzo na Kipanga bado wana alama sawa 23, Mafunzo wakibaki nafasi yao ya saba (7) na Kipanga wapo  nafasi nane (8)
Katika mtanange huo Wazee wa jelajela Mafunzo wamevaa jezi za njano na Majeshi wa Kipanga  wamevaa jezi za blue.

No comments: