Sunday 20 March 2016

Manahodha nje debi ya Manchester.


Mashabiki wa soka ya Uingereza leo wataelekeza macho yao kwa debi ya Manchester katika Ligi Kuu ya Uingereza.
Mechi hiyo itachezewa uwanja wa Etihad.
Klabu zote mbili zitakuwa bila manahodha wake, Vincent Kompany (City) na Wayne Rooney (United) ambao wanauguza majeraha.
Kompany aliumia tena mguuni wakicheza dhidi ya Dynamo Kiev Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katikati ya piki.
Uamuzi kuhusu beki mwenzake Nicolas Otamendi, aliyeumia pia wakati wa mechi hiyo, utafanywa kabla ya mechi.
Upande wa United, kuna shaka kuhusu Ander Herrera anayetatizwa na jeraha la mtoki ambaye pia alikosa mechi ya Europa League dhidi ya Liverpool.
Ashley Young na Cameron Borthwick-Jackson wamerejea mazoezini baada ya kuuguza majeraha na huenda wakachezeshwa.
Debi ya leo ndiyo ya 171 ya Manchester na iwapo City watashindwa basi matumaini yao ya kushinda taji ni kama yatakuwa yamefutika.
United wanatazama debi hiyo kama fursa inayoweza kuwapa matumaini ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Majuzi, meneja wa United Manchester United Louis van Gaal alisema: "Natumai City itakuwa kichocheo. Tunahitaji kulaza City na tuna matumaini bado ya kufuzu [kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya]”.
City wamo nambari nne na alama 51 nao United nambari sita na alama 47.
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema debi huwa hatari sana na hawataki kupoteza alama.
Manchester City wameshinda debi nne kati ya sita za Manchester walizocheza majuzi zaidi ligini, ingawa walizoshindwa ndizo mbili za karibuni zaidi.
Mechi za Jumapili Ligi Kuu ya Uingereza (saa za Afrika Mashariki)
  • Newcastle v Sunderland 16:30
  • Southampton v Liverpool 16:30
  • Man City v Man United 19:00
  • Tottenham v Bournemouth 19:00
  • bbc.

No comments: