KAMPENI “FICHUA VIPAJI"
Masikio na macho wa wazanzibar yanatamani kusikia na kuona siku moja Zanzibar ikitajwa
kitaifa na kimataifa kukua kisoka kama zilivyonchi nyengine ambazo leo hii zikitajwa
tu, kitu cha mwanzo watu watasifu kwa kiwango chao cha soka ni kama Brazil, Ujerumani,
Uingereza na kwengineko.
Wengi sana wanajiuliza, ni kwanini wao waweze sisi tusiwese? Maswali
haya ni mengi kwa mashabiki wa soka nchini mwetu lakini kwa ujumla hakuna alieambulia
jibu zuri la suala hilo kila mmoja abakia na jibu lake likiwa ndilo au silo
sawa tu.
Kwakua mimi mwenyewe ni mdau wa soka nambari one niliamua
moja kwa moja niingie katika mchakato wa kutazama ni kwanini hasa wazanzibar
leo hii tumekua nyuma katika soka ingawa ni nchi ndogo kigeographia na hata kiuchumi,
lakini waswahili wanamsemo wao mashuhuri kabisa “mtu hujikuna ajipatapo”
viwanja hivyohivyo tulivyonavyo mbona vinachezeka tu na kua na mafanikio,kwanini
kwetu mafanikio ni kama Ngamia kupenya katika tundu ya Sindano?
Baada ya kuingia ndani kabisa kutazama nini chanzo hasa siku
zote tuwe mkiani katika mashindano mengi ya soka , kitu cha kwanza kabisa
tuligundua ni “SIASA’ ndio iliyotuharibia wazanzibar! asilimia sabiini (70%) ya
wazanzibar maisha yao ni siasa tena imepenya katika kila kona ya michezo hapa
nchini.
Tafiti hii ndogo imegundua
kua, hata viongozi wa soka katika mamlaka husika wanaongozwa na siasa kiasi
ambacho hata maamuzi yao pia hutoka kisiasa saisa ya kugawanyika kwa mapande, hivi
hapa kweli pana maendeleo katika jamii kama hii ya uongozi?
Mbona kwa wenzetu pia siasa ipo lakini haikua kama
tulivyosisi, mfano mzuri hapo Kenya tu wala sio mbali nasisi, wanasiasa kama
sisi, ni waafrika kama sisi, hata uchumi wao hatujapishana kiasi hicho lakini
mara nyingi wamekuwa wakitupiga bao kila siku tuchezapo nao hapa sitaki
nielezee sana mana mifano ipo mingi na wa mwisho juzi tu katika Kombe la
Mapinduzi Cup kwa macho mawili imeshuhudiwa Kenya ikiondoka na kikombe wazanzibar
wenyewe tukiwa tumetumbua macho tu tena tukisherehekea ushindi wa wenzetu,si
vibaya kufurahia mafanikio ya mwenzako lakini ni aibu iliyoje kwa wenyeweji
tena kombe lenyewe la mapinduzi yaliyoleta usawa kwa waafrika wa kizanzibar
kushindwa nyumbani kwao.
Niliamua kutafuta wadau wa soka kuona jee kuna uhalisia
wowote juu ya tafiti hii,wamwanzo kabisa niliekutana nae alikua alikua ni mchezaji
wa Polisi Mara daraja la kwanza Danny
Manyenye.
Alisema wadau wa soka nchini wanatakiwa kupunguza au
kuondosha kabisa “SIASA” katika medani za soka ili kuruhusu vipaji vya
wachezaji kukua “viongozi wa soka nchini wamekua washabikiaji wa siasa mpaka
huiingiza katika soka hivyo hupelekea kukinzana baadhi ya mitazamo baadae hutofautiana wao kwa wao hatime
kutokua na maendeleo katika timu husika.”
Aidha alisema kuwa nchi ina vipaji vingi sana mitaani lakini
wanaotakiwa kuviendeleza hawaonekani na badala yake wanasubiri kumuona mchezaji anatoka chini
mwenyewe kwa nguvu zake na anaposhindwa kutoka ndio humalizika kabisa kisoka
lakini kama viongozi wanakua makini na ukuzaji wa vipaji vingezalishwa vingi tu
sio kama sasa nchi inakosa dira kisa siasa.
Mwengine ambae hakupenda jina lake liandikwe amekubalina moja
kwa moja na hoja kua siasa ndio sababu kuu inayopelekea soka letu wazanzibar
kuwa chini, amesema ingawa zipo sababu nyengine nyingi lakini ni ndogondogo kubwa
zaidi ni siasa.
“hata mgogoro wa sasa unaousikia ZFA huwenda ikawa kuna kitu
katikati ambcho ni siasa,kwa kweli wazanzibari sisi tumuombe mungu sana lakini sijui tunakwenda wapi”alisema
Wazanzibar siku zote wanatamani kusikia wapo juu kisoka
ukweli vipaji vipo tele mitaani lakini kama siasa isipotazamwa kwa makini zaidi
wazanzibar tutaishia hapahapa kukaribisha watu na kusindikiza wat utu.
No comments:
Post a Comment