Monday, 14 March 2016

UBINGWA WAHAMIA KWA PSG UFARANSA


Paris St-Germain wametangaza ubingwa wa ligi ya Ufaransa ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya ligi kumalizikabaada ya kuisambaratisha Troyes kwa bao 9-0 huku Zlatan Ibrahimovic akiweka bao nne kambani kuimaliza timu hiyo inayobuuza mkia kwenye msimamo wa ligi.
Edinson Cavani, Javier Pastore na Adrien Rabiot kila mmoja alipasia nyavu na kuipa PSG magoli 3-0 ya kuongoza ndani ya dakika 19 nza kwanza kabla ya Ibrahimovic kupiga bao tatu ndani ya dakika 10 za kipindi cha pili.
Matthieu Saunier alijifunga huku Cavani akirudi tena wavuni kufanya matokeo kuwa 8-0 kabla ya Ibrahimovic hajakamilisha bao lake la nne.
Wamewezaje kunyakua ubingwa mapema?
Vijana na Laurent Blanc wananyanyua ndoo ya nne mfululizo kwa style ya aina yake baada ya ushindi mzito wa kihistoria kwenye mechi yao ya ugenini kwa kuifunga Troyes magoli 9-0.
Wameweza kufanya hivyo wakiwa wamepoteza mchezo mmoja pekee katika mechi 30 za ligi walizocheza, walipoteza kwa kichapo cha bao 2-1 dhidi ya Lyon mwezi February. PGS wana wastani wa magoli 62 ya kufunga na kufungwa wakiwa wameruhusu nyavu zao kucheza mara 15.
Wameshinda mechi 24 kati ya 30 wakati huo Ibrahimovic akiwa amefunga magoli 31 kwenye mechi 25 alizocheza akifuatiwa na Cavan mwenye magoli 16 katika mechi 27.
Rekodi muhimu
  • Paris St-Germain inafanikiwa kutwaa taji la ligi zikiwa zimesalia siku 62 wakati huo zikiwa zimesalia mechi nane, rekodi ambayo haijawekwa na timu yoyote kutoka ligi tano kubwa za barani Ulaya.
  • Katika michezo 115 ya Ligue 1 ambayo Zlatan Ibrahimovic amecheza, amefunga magoli 102 na ku-assist magoli 35.
  • Ushindi huo ni wa sita msimu huu kwa PSG kufunga magoli manne au zaidi kwenye mechi moja ya Ligue 1.
  • Taji hilo ni la sita kwa PSG na la nne mfululizo kwenye ligi.

No comments: