Tuesday, 1 March 2016

WACHEZAJI WAPO, VIPAJI VIPO LAKINI WATACHEZAJE VIZURI WAKATI HATA PESA YA KUNUNULIA KIATU HAWANA.




Wachezaji wadogowadogo wa mpira wa miguu nchini wameshauriwa kufanya jitihada kubwa katika soka ili kuhakikisha wanashinda changamoto zilipombeleyao hatimae waonekane katika ngazi ya taifa hata kimataifa.

Ushauri huo umetolewa leo na beki nambari mbili wa timu ya Sabasaba United ligi daraja la pili  morogoro Said Daz Alvenga alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA.

Akizungumzia changamoto zinazowakumba wachezaji wadogowadogo katika soka amesema kwanza kabisa wachezaji wadogowadogo wapo  wengi sana hivyo mpaka utoke kisoka basi lazima ufanye juhudi kubwa.
Amesema mchezaji  anakwenda kwenye timu anakuta wapo wachezaji takriban 50 na mwalimu anataka watu 20 wenye muelekeo mzuri, hivyo mpka uwemo katika wachezaji hao mchujo unakua mkubwa sana, kipaji chako na bidii yako ndiyo pekee itakayokufanya utazamwe.

Akiendelea kueleza changamoto zinafowafika  Alvenga amesema, wachezaji wadogowadogo wanakabiliwa na changamoto nyingi sana  ikiwa ni pamoja na kukosa huduma muhimu katika utendaji kazi.

Amesema mchezaji anaweza kwenda mazoezini lakini anaporejea  nyumbani wakati mwingne hajui hata anakula nini  kutokana na hali ya maisha ilivyongumu.

Daz Alvenga anasema “kwa mfano mimi mwenyewe naweza kwenda mazoezi  lakini  ninaporudi nyumbani wakati mwingne sijui nakula nini kutokana na hali ya maisha ninayoishi , pia napata wakati mgumu sana wakati  viatu vyangu vinapoisha maana sina uhakika wa kupata viatu vyengine kwa wakati, huwa napumzika tu nyumbani.”alisema Daz Alvenga


Ametoa wito kwa wahisani na wadau wa mpira wajitokeze kwa wingi katika kuwadhamini wachezaji wadogowadogo akisema  Tanzania ina vipaji vingi lakini wengi wao  huishia mitaani tu kwa sababu ya kukata tamaa kutokana na mazingira magumu wanayokutana nao katika soka.

No comments: