
Mashabiki wa Kobe Bryant watengezewa bidhaa maalum za spoti
kwa ajili ya kumbukumbu ya nyota huyo NBA
Mashabiki wa mpira wa kikapu na wapenzi wa nyota wa L.A
Lakers Kobe Bryant, wametengezewa bidhaa maalum za spoti kwa ajili ya
kumkumbuka mchezaji huyo baada ya kustaafu.
Bidhaa hizo zilizochapishwa nambari 24 inayoashiria jezi
aliyokuwa akivaa Kobe Bryant wakati wa uchezaji wake, zitauzwa kwa bei
inayofikia hadi dola 38,000.
Miongoni mwa bidhaa hizo ni kama vile kofia,flana na koti
ambayo yataanza kuuzwa rasmi kuanzia wiki ijayo baada ya Kobe Bryant kustaafu
rasmi.
Wiki ijayo, Kobe Bryant atachezea L.A Lakers mechi yake ya
mwisho ya NBA dhidi ya Utah Jazz katika uwanja wa Staples Center. Bei ya tiketi
za mechi hiyo itaanzia dola 670.
No comments:
Post a Comment