
Licha ya mchezo huo
kuchezwa katika hali ya mvua lakini boy’s walijipatia bao la mapema
lililofungwa na Abrahman Othman katika dakika ya 16, ambalo lilikuwa ni bao
pekee katika mchezo huo lililoweza kuwapatia boy’s alama tatu za mchezo.
Katika dakika ya 74
mlinda mlango wa Jang’ombe boy’s Ali Yussuf alimfanyia faulu mchezaji wa KVZ
Nassir Bakar ndani ya boks, na ndipomwamuzi wa mtanange huo aliamuru kupigwa
kwa mkwaju wa penalt, lakini mchezaji wa KVZ Suleiman Ali aliikosa penalt hiyo
baada ya mlinda mlango Nassir kuutoa mpira huo.
Akizungumza na SALMA
SPORT’S MEDIA kocha wa Jang’ombe boy’s Issa Othman Amasha ambae wameibuka na
ushindi huo licha ya kushinda lakini amesema kuwa tatizo la ufungaji bado lipo kwa
wachezaji wake. “Tatizo la ufungaji bado lipo lakini sasa, leo siwezi kulaumu
sana kwa sababu mpira wenyewew ulikuwa ni wa mvua”. Alisema kocha Amasha.
Lakini kocha wa timu ya
KVZ Othman Hassan King, amesema hali ya hewa ndio iliyosababisha mechi kuwa
ngumu kwao.
“Mechi ya leo kutokana na
hali ya hewa, kidogo imesababisha mechi hii kubadilika kutokana na hali ya
hewa, na hali ya hewa ndiyo iliyosababisha kuleta ugumu katika timu yangu”. Alisema
kocha King.
KVZ bado wamesalia
nafasi yao ya pili wakiwa na alama 33,
na Jang’ombe bpy’s sasa wapo nafasi ya kumi 10 na alama 22.
No comments:
Post a Comment