Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU imezidi kujiweka kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya jana kuwanyuka majeshi wa Kipanga bao 1-0 katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa mjini Unguja.
Katika mchezo huo JKU
hawakucheza vyema licha licha ya ushindi huo walioupata kwa penalt baada ya
vuta nukuvute katika lango la Kipanga wakati JKU walipotaka kufunga bao, ndipo
mwamuzi wa mtanange huo Issa Haji alipoamua ipigwe penalt.
Feisal Salum ndipo
alipopiga penalt hiyo na mpira moja kwa moja kuingia wavuni katika dakika ya 79
ya mtanange huo.
JKU bado wanaendeleza
ubabe wao wakiwa na alama 47, huku wanaowafukuzia ni timu ya KVZ ambayo wapo
nafasi ya pili na alama 33, Kipanga wao wana alama 24 wakiwa nafasi ya nane 8.
No comments:
Post a Comment