Katika mtanange huo
Miembeni walianza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Ramadhan Hamza Kidilu
katika dakika ya saba 7, Kidilu akarudi tena nyavuni mnamo dakika ya 16 kwa
kuipatia Miembeni bao la pili.
KMKM walianza kupachika
bao la kwanza kupitia mchezaji Haji Simba katika dakika ya 20, na dakika ya 34
Makame Haji Mngwali akaipatia KMKM bao la kusawazisha.
Timu hizo hadi
zinakwenda mapumziko, zilikuwa sare ya mabao 2-2.
Kuanza kipindi cha pili
tu katika sekunde ya 10, Faki Mwalim akapachika bao la tatu, na dakika ya 50
Faki Mwalim akarudi tena kwa kumaliza karamu hiyo ya mabao, na mchezo huo
ukamalizika kwa KMKM kuibuka na ushindi mnene wa mabao 4-2 dhidi ya Miembeni.
KKMKM sasa wanashika
nafasi ya pili wakiwa na alama 33, Miembeni wapo nafasi ya sita 6 na alama 30.
No comments:
Post a Comment