Rais UEFA Michel Platini atangaza mpango wa kuachia ngazi kufuatia msimamo wa CAS
Rais wa UEFA Michel
Platini ametangaza mpango wa kutaka kujiuzulu kufuatia uamuzi wa mahakama ya
kimataifa ya soka CAS iliyompunguzia adhabu yake kutoka miaka 6 hadi 4.
Mawakili wa Platini
walitoa maelezo na kuarifu mpango huo wa rais wa UEFA baada ya CAS kutoa uamuzi
kuhusiana na adhabu yake.
Licha ya uamuzi wa CAS,
Platini alisisitiza kuendeleza kesi hiyo kwenye mahakama za soka za Uswisi.
CAS iliamua kumpunguzia
Platini adhabu ya kufungiwa kujihusisha na soka kutoka miaka 6 hadi 4 na faini
ya fedha kutoka Franc 80,000 hadi 60,000.
Platini alitangaza
kuweza kujiuzulu kutoka kwenye nafasi yake ya urais wa UEFA endapo mahakama ya
CAS itakataa kufutilia mbali adhabu hiyo.
Rais wa zamani wa FIFA
Sepp Blatter pia aliwahi kufungiwa miaka 8 na kutozwa faini ya fedha Franc
milioni 2 kufuatia sakata la ufisadi lililokuwa likiwakabili.
No comments:
Post a Comment