“Ingawa changomoto ni nyingi sana lakini nipambana kwa hali
na mali mpaka kuona nafanikiwa katika kuyafikia malengo niliyojipangia katika
maisha yangu ya soka.”
Hayo ni maneno ya mchezaji wa timu ya Villa United FC ya
visiwani Zanzibar inayo wania nafasi ya
kuingia 8 bora Juma Yusuf (James) wakati alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S
MEDIA leo hii juu malengo ya kuwatazama
wachezaji wenye nia ya kufika mbali
katika soka.
Mchezaji huyo amekua tegemezi kubwa katika timu yake hiyo
kutokana na juhudi za makusudi anazozifanya katika kukuza soka la nchi nayeye
mwenyewe.
James amesema mwenye umri wa miaka kumi na saba (17) ameamua
kufanya jitihada kubwa ya mazoezi na kuiga kwa wachezaji wa kimataifa namna ya
uchezaji wao ili nae siku moja acheze soka nje ya nchi kwa lengo la kuliletea
sifa taifa lake kama ilivyo kwa mataifa mengine.
Amesema katika kuyafikia malengo yake hayo amekua
akikabiliana na changamoto nyingi sana ambazo kwa namna moja ama nyengineyo
kama mtu hatokua makini zinaweza kumrudisha nyuma na kufeli.
Amezitaja changamoto hizo ni pamoja kujiunga kwenye timu
ukawa unafanya vizuri lakini kwa uzuri wako hatimae ukaanza kusemwa ukaambiwa
hufai na kukukata tamaa kwa makusudi wakati sio uhalisia ulivyo kumbe ni roho
mbaya tu zilizojengeka kwa baadhi wa wadau na viongozi.
Akijibu suala la mwandishi wa habari SALMA HASSAN kua
analizungumziaje suala la vipaji kutojaliwa na kuthaminiwa amesema vipaji nchini mwetu vimo tena vingi sana
lakini tatizo liliopo ni kua havizingatiwi wala havithaminiwi na badala yake vinaachwa vikifa vijijini.
Sambamba na hayo James ametoa wito kwa wadau wa soka na
wahisani kwa ujumla kuwawezesha wachezaji wadogo wadogo kwani wanauwezo wa
kutosha katika soka lakini wanashindwa kuonekana kutokana na kutowezeshwa.
Pia amemalizia kutoa ushauri kwa wachezaji wenzake ambao
wanamalengo kama yake kujituma katika mazoezi na kutovunjika moyo kirahisi pia
kuwasikiliza walimu wao vipi wanavyowaelekeza na kutumia mafunzo hayo kama
inavyotakiwa.
No comments:
Post a Comment