Wednesday, 24 February 2016

MESSI AVUNJA REKODI YA PETR CECH

Lionel Messi alipiga bao mbili kwenye mchezo wa Champions League hatua ya 16 bora dhidi ya Arsenal usiku wa Jumanne February 23 kwenye dimba la Emirates, London.
Endapo Arsenal itashindwa kufuzu kwa hatua inayofuata itakuwa imeondoshwa kwenye michuano hiyo kwa mara ya sita mfululizo katika hatua ya 16 bora. Ili Arsenal iweze kusonga mbele kwenye mashindano hayo makubwa Ulaya kwa ngazi za vilabu, inatakiwa kuibuka na ushindi wa bao 3-0 kwenye uwanja wa Now Camp.
Rekodi ya Arsenal kwenye michuano ya Champions League hatua ya 16 bora tangu msimu wa 2010-11.
2015-16 – Lost 2-0 (mchezo wa kwanza, unasubiriwa mchezo wa marudiano)
2014-15 – Lost 3-3 (away goals) to Monaco
2013-14 – Lost 3-1 to Bayern
2012-13 – Lost 3-3 (away goals) to Bayern
2011-12 – Lost 4-3 to Milan
2010-11 – Lost 4-3 to Barcelona.
Rekodi muhimu baada ya mchezo wa kwanza Arsenal vs Barcelona (Emirates Stadium)
  • Messi alikuwa hajamfunga Petr Cech kwa muda wa saa 10 na dakika 11 ambazo amecheza uwanjani (mechi saba).
  • Messi sasa amefikisha magoli nane kwenye michuano ya UEFA Champions League dhidi ya Arsenal pamoja na AC Milan ambayo amezifunga timu hizo.
  • Ilimchukua sekunde 47 tu tangu Mathieu Flamini aingie uwanjani akawa amesababisha penati.
  • Barcelona haijapoteza mchezo kwenye mechi 33 za mashindano rekodi nzuri kuwahi kutokea kwenye timu hiyo. Reodi ya kucheza mechi nyingi bila kupoteza kwa timu za Hispania inashikiliwa na Real Madrid ambayo haikupoteza katika mechi 34 msimu wa mwaka 1987-88.
  • Arsenal imeshindwa kufunga goli kwa mara ya kwanza kwenye mechi 14 za Champions League.

No comments: