Wednesday 24 February 2016

Golden State Warriors yaweka historia ya ushindi NBA

Mabingwa watetezi wa taji la NBA Golden State Warriors, wameweka historia kwa kuwa timu ya kwanza kuweza kushinda mechi 50 ndani ya kipindi kifupi kwa msimu mmoja.
Golden State Warriors iliandikisha historia hiyo katika NBA baada ya kuishinda Atlanta Hawks 102-92 hapo jana katika uwanja wa Philips Arena.
Hadi kufikia sasa, Golden State Warriors imeweza kushinda jumla ya mechi 50 kati ya 55 walizocheza msimu huu kwenye ligi kuu ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani.
Timu hiyo iliyoanza kwa kasi msimu huu baada ya mafanikio makubwa msimu uliopita, inatarajiwa kuendeleza mafanikio yake kwa usaidizi wa wachezaji wake wakali kama vile Stephen Curry.

No comments: