Monday 29 February 2016

OSCAR: MAKOCHA ACHENI UBINAFSI


 Baadhi ya walimu wa timu za mpira wa miguu nchini(makocha) wanadaiwa kua na tabia mbaya ya ubinafsi kwa baadhi ya wachezaji na hatimae kuwavunja moyo wachezaji hao wanaocheza kwa ari ya maendeleo ya kukuza vijapi vyao.

Kauli hiyo imetolewa leo hii na OTHMAN OSCAR mchezaji wa timu ya  Jamhur  ya Makunduchi  daraja la pili taifa anaechezea timu hiyo nambari  saba (7) wakati alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA wakati walipokua wakijadili changamoto mbalimbali zinazolikumba soka la Zenj na wachezaji kwa ujumla.

Amesema soka la Zenji  ni zuri  lakini kuna vitu vinarudisha nyuma ikiwamo walimu wa timu zenyewe baadhi yao ni wabinafsi kiasi ambacho mchezaji anaweza akacheza kwa kiwango kizuri lakini akashindwa kuthaminiwa  na wakati mwengine wachezaji  wanaotazamwa kwa mtindo huo na walimu huwenda hata mechi asichezeshwe kwasababu tu zakibinafsi alizonazo mwalimu huyo.

“unaweza ukacheza timu kubwa ikawa kiwangochako kipo poa  sana lakini makocha wanaubinafsi akawa hakuchezeshi pasipo na sababu yoyote ile”alisema Oscar.


Oscar amemalizika kwa kutoka wito kwa makocha wote wa Zanzibar  akiwataka kuwa makini na kazi zao na kuacha ubinafsi  kwani timu nyingi zinakosa kuimarika kwasababu  ya makocha kua na tabia hiyo.

No comments: