Monday 29 February 2016

HENRY HAJAACHA KUMSIFIA RASHFORD, NA HILI NDIYO NENO LAKE



Thierry Henry ametoa pongezi za dhati kwa kinda wa Manchester United Marcus Rashford, baada ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu nchini Uingereza na kuonesha kiwango cha hali ya juu.
Mshambuliaji huyo alianza katika mchezo wa jana dhidi ya Arsenal uliopigwa Old Trafford, na kufanikiwa kuweka kambani mabao 2 katika ushindi wa mabao 3-2, huku pia akifanya hivyo katika mchezo wa ligi ya EUROPA dhidi ya klabu ya FC Midtjylland Alhamisi wiki iliyopita.
“Ninachopenda kutoka kwake ni kwamba, amefunga magoli manne katika mechi mbili, namna anavyoendana na kasi ya mchezo, namna anavyoupokea mpira, kuna vitu pale naviona,” Henry alisema.
“Uelewa wake, akiwa ndani ya eneo la hatari, utulivu wake. namna anavyojiweka langoni mwa timu pinzani, uwezo wake mkubwa wa kupiga mipira ya kichwa ambayo inalenga lango. Lakini bila ya kusahau pia anafanya kazi ya kuharibu mashambulizi ya timu pinzani”.

No comments: