Wadau wa soka nchini watakiwa
kujitokeza kwa wingi kudhamini ligi pamoja na timu za mpira nchini ili kunusuru
vipaji vya wachezaji na hatimae kufikia maendeleo ya soka yanayotarajiwa.
Kauli hiyo imetolewa na mchezaji
wa timu ya KMC ya Kinondoni Dar es Salaam iliyopo daraja la kwanza Timamu
Maarifa wakati alipokua akizungumza na salma sport’s media katika mtazamo wake
wa soka la Tanzania.
Amesema soka ni zuri na lipo
lakini bado kuna changamoto ni nyingi
zinazolikumba soka la Tanzania ikiwemo uchumi mdogo kwa timu nyingi hatimae
kutowatia moyo wachezaji ambao kwa ujumla wanategemea soka kama ni maisha yao.
Maarifa amesema “timu nyingi
hazina uwezo wa kifedha zinasumbua kuwalipa wachezaji wakati wachezaji
wanahitaji kulipwa vizuri lakini pia uwongozi mbaya kwa timu zetu hizi, yaani wasimamizi wa soka sometime
wanafeli”alisema Maarifa.
Amesema ili kuwasaidia wachezaji
na timu basi ni vyema kwa timu hizo watafute wadhamini kwani kampuni zipo nyingi zinazoweza kujitolea
kudhamini timu, ingawa baadhi ya makampuni mengine yanakua wagumu kudhamini ni
vizuri kufanya jitihada za kuwashawishi mpaka wakubali.
Pia ametoa wito kwa viongozi wa
timu waache ubabaishaji waweke kando
mambo yao binafsi na hapo ndipo mambo yatakapokwenda vizuri.
Mbali na wito huwo kwa viongoz
lakini pia amewashauri wachezaji kuwa wavumilivu kwa sababu mchezaji anaweza
kua na unauwezo mzuri wa kucheza ila
ikawa si chaguo la mwalimu na ukashindwa kupata nafasi lakini uvumilivu ndio ushindi.
No comments:
Post a Comment