Na: Abubakar Khatib (Kisandu) Zanzibar.
Mkutano mkuu wa dharura wa ZFA TAIFA umehitimishwa jioni ya
leo hii ambapo wajumbe wameamua maamuzi mazito katikamkutano huo.
Ajenda tatu zilijadiliwa katika mkutano huo ambao umefanyika
katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Kikwajuni Mjini
Unguja ambapo miongoni mwa mada tatu zilizojadiliwa, moja ni kujadili mwenendo
wa kamati tendaji ambapo muwasilishaji wa mada hiyo alikuwa Makamu wa Urais ZFA
Unguja Haji Ameir (Mpakia) ambae hakuonekanwa katika mkutano huo na mada yake
hiyo ikawasilishwa na Makamu wa Urais ZFA Pemba Ali Mohammed.
Baada ya kusikiliza mada hiyo wajumbe 50 waliokuwepo kwenye
ukumbi huo baada ya kuisikiliza mada iliyowasilishwa ambapo wamekubaliana
kupiga kura, kura ambayo ilikuwa inamuhusu Makamu wa Urais Unguja Haji Ameir
aliepeleka kesi ya soka Mahakamani mwishoni mwa mwaka 2014 ambapo wajumbe
walitaka afukuzwe kwenye chama hicho na asijihusishe na mambo ya michezo kwa
muda wa miaka 4.
Wajumbe 50 wakapiga kura ambapo wajumbe 43 walisema afukuzwe
na wajumbe 4 walisema asifukuzwe ambapo wajumbe 3 hawajapiga kura.
Hivyo Alhaj Haji Ameir ambae ni Makamu wa Urais ZFA Unguja
amefutwa rasmi nafasi hiyo na kutojishughulisha na mambo ya michezo kwa muda wa
miaka 4.
Aidha mkutano huo umeiondoa kamati ya muda iliokuwa ikiongoza
soka la Zanzibar ambapo wajumbe 42 walisema kuwa kamati hiyo iondoke na wajumbe
6 walisema wasiondoke wakati wajumbe 2 kati ya hao 50 hawajapiga kura.
Ajenda ya pili iliyowasilishwa katika mkutano huo kuhusu
kuteuliwa Mkaguzi wa Mahesabu yaani 'Auditors' kwa ajili ya kuvipitia vitabu
vya mahesabu vya Chama hicho ambapo mkutano huo umekubaliana kuchaguwa Kampuni
yenye sifa kufanya ukaguzi wa Mahesabu kwa ZFA Taifa ambapo utafanyiwa tangu
uongozi wa ZFA wa mwaka 2012 hadi 2016, yani kipindi cha Rais Amani Makungu na
Ravia Idarous Faina wa sasa.
Na ajenda ya tatu mkutano mkuu ulikuwa unatakiwa kuamua
kuteuwa wajumbe 5 watakaoandika upya Katiba ya ZFA ambapo wajumbe 5
walioteuliwa kati ya 12 waliopendekezwa Awali ni Eliud Peter Mvella kura 46
(Msaidizi mkurugenzi TFF na Mwanasheria), Saleh A. Said kura 43 (Wakili upande
wa ZFA), Affan Othman Juma kura 42 (Kiongozi wa mpira na taaluma ya sheria) Ame
Abdalla Dunia kura 40 (Mwalimu/Taaluma ya Sheria), na Othman Ali Hamad kura 36
(Mwanasheria, Kiongozi na mchezaji wa mpira).
Aidha mkutano huo umehalalisha wajumbe waliokuwepo kwenye
ZFA Wilaya ya Magharibi “B” kuwa ni halali na wanatambuliwa na mkutano mkuu na
hautofanyika tena uchaguzi kwenye Wilaya hiyo.
Kuhusu uchaguzi wa ZFA Taifa mkutano huo umetowa tarehe ya kufanyika
Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika April 9, 2016 huko Kisiwani Pemba
ambapo nafasi ya Urais, Makamu Urais Pemba na Makamu Urais Unguja ndizo nafasi
tatu zitagombaniwa katika uchaguzi huo ambapo pia katiba itakayotumika ni ya
mwaka 2010.
Jambo jengine katika mkutano huo ni Ligi kuu soka Zanzibar
kanda ya Unguja ambayo imeendeshwa na Kamati ya Mpito iliofutwa leo hii, kwa
makubaliano ya mkutano huo ligi hiyo wamesema ni halali na wanaikubali, na ligi
kanda ya Pemba karibuni itaanza kuchezwa baada ya kukaa kamati tendaji.
Katika mkutano huo Makamu wa Urais Unguja Haji Ameir
hakuonekanwa ambapo Kijana Ramadhan Muhsin amekamatwa na Jeshi la Polisi baada
ya kwenda kwenye mkutano huo akiwa si mjumbe wala si mualikwa huku akivaa
kitambulisho cha Makamu wa Urais Unguja yani Haji Ameir.
1 comment:
Tumechoka na migogoro ya ZFA.
Post a Comment