Bayern Munich imepambana kutoka nyuma kwa goli 2-0 hadi
kuichapa Juventus kwenye dakika za nyongeza na kusonga mbele kwenye hatua ya robo
fainali ya Champions League.
Timu hizo zilitoka sare ya kufunga kwa bao 2-2 kwenye mchezo
wa kwanza, Paul Pogba na Juan Cuadrado wakaifungia Juve na kuiweka mbele kwa
bao 2-0 dhidi ya Bayern kwenye mchezo wa jana usiku.
Robert Lewandowski alipiga bao kwa kichwa na kufufua matumaini
ya Bayern kubadili matokeo kabla ya Juve kumruhusu Thomas Muller kusawazisha
katika dakika ya mwisho na kuufanya mchezo kuwa sare ya magoli 2-2 na
kulazimisha timu hizo kwenda kwenye dakika za nyongeza.
Bayern wakafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya
kwa style ya aina yake baada ya Thiago na Kingsley Coman kuifungia timu yao
mabao mawili katika muda wa nyongeza. Mchezo huo ukamalizika kwa Bayern
kuichapa Juve magoli 4-2 na kufanya jumla ya magoli yote ya michezo miwili kuwa
Bayern 6-4 Juve.
Juve ambao walitawala mchezo kwa asilimia nyingi za muda wa
kawaida walichanganywa na goli la kusawazisha la dakika za lala salama la
Muller pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Guardiola ya kuwaingiza Coman na
Thiago ambao waliamua mchezo.
Mbali na kupoteza mchezo huo, kinachowaumiza zaidi Juve ni
goli lilifungwa na Coman mchezaji wao kinda ambaye yupo Bayern kwa mkopo wa
muda mrefu.
Kijana huyo wa kifaransa mwenye miaka 19, ali-assist magoli
matatu wakati Bayern inashinda bao 5-0 dhidi ya Werder Bremen kwenye mchezo wao
wa ligi weekend iliyopita na alikuwa kwenye kiwango bora baada ya kuingia
kuchukua nafasi ya Xabi Alonso.
Shaffih Dauda.
No comments:
Post a Comment