Arsenal hawajafika robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
tangu 2010
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini vijana wake
walicheza vyema uwanjani Nou Camp licha ya kulazwa 3-1 na Barcelona Ligi ya
Klabu Bingwa Ulaya.
Arsenal walilazwa kupitia mabao ya Neymar, Luis Suarez na
Messi. Bao lao la kufutia machozi lilifungwa na Mohamed Elneny.
Arsenal hawajafika hatua ya robofainali Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya tangu 2010.
"Nafikiri tulicheza vyema, ulikuwa mchezo mzuri kati ya
timu mbili nzuri. Tumeondolewa kwa masikitiko lakini wana ustadi wa hali ya juu
hasa katika safu ya mashambulizi na ukifanya kosa kidogo tu safu yako ya ulinzi
wanaweza kukuadhibu,” alisema Wenger baada ya mechi.
"Wakati muhimu katika mchezo huo ni mambo yalipokuwa 1-1
kwa sababu nilidhani walikuwa wanayumbayumba kiasi. Kama tungefunga bao la pili
wakati huo badi mambo yangekuwa tofauti labda. Lakini hatukuweza.
"Katika michezo yote miwili, ukiangalia nafasi ambazo
tuliunda, zilikuwa nyingi. Inauma kuondolewa kwenye michuano lakini tulicheza
vyema sana dhidi ya timu ambayo labda ndiyo bora zaidi Ulaya.”
Arsenal walilazwa 2-0 mechi ya mkondo wa kwanza uwanjani
Emirates, mabao yote yakifungwa na Lionel Messi.
Arsenal sasa watajaribu kufufua kampeni yao msimu huu kwa
mechi ugenini Goodison Park dhidi ya Everton Jumamosi.
Barca, watakaokutana na Villa Real ligini Jumapili, watajua
mpinzani wao robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Ijumaa droo itakapofanywa
mjini Nyon, Uswizi.
BBC.
No comments:
Post a Comment