Timu ya Mkungu Malofa jana iliizuia timu ya Chuo/Basra kukata
tiketi ya kucheza ligi ya Zanzibar baada ya kuinyuka kwa bao 1-0 katika mchezo
wa ligi daraja la Kwanza taifa Pemba hatua ya 6 Bora ulipchezwa jana katika
uwanja wa Gombani.
Katika mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wengi timu
ya Chuo/Basra ingefanikiwa kushinda ingalikuwa ya kwanza kupanda daraja kwa
kufikisha alama 9, na sasa itahitaji kushinda mchezo wake wa mwisho hapo kesho
na timu ya Danger Boys.
Goli pekee la Mkungu Malofa lilifungwa katika dakika ya
kwanza ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Abdalla Moh`d (Mbongo).
Mchezo huo ambao ulichezeshwa na mwamuzi Faki Khatibu kutoka
Wilaya ya Mkoani timu ya Chuo/Basra ilionyesha kutoridhika na baadhi ya maamuzi
ya mwamuzi huyo jambo ambalo lilipelekea mashabiki wake kutoa maneno ya kashfa
kwa mwamuzi huyo.
KWENGINEKO
Katika mchezo mwengine timu ya New Star iligawana alama 1-1
baada ya kutoka sare ya kufungana goli 1-1 katika mchezo uliochezwa wakati wa
saa nane za mchana uwanjani hapo.
Leo kutakuwa na mchezo katika ya timu ya Wawi Star na Danger
Boys katika uwanja wa Gombani wakati wa saa 10 jioni mchezo ambao unategemewa
kuwa wa ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji nafasi ya kuingia
katika timu tatu zitakazopanda daraja.
Ligi hiyo hadi sasa inaongozwa na Wawi Star yenye alama 7
baada ya kucheza michezo mitatu, Chuo/Basra alama 6 imeshacheza michezo mine,
Mkungu Malofa inashika nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 5 na imeshacheza
michezo mine.
Timu za Danger Boys, Maji maji na New Star zote zina alama 4
kila moja, hivyo kufanya hadi sasa timu zikibakiwa na mchezo mmoja mmoja
kutokuwepo na timu iliyojihakikishia kupata nafasi ya kupanda daraja.
No comments:
Post a Comment