Shirikisho la kandanda duniani la FIFA limetoza faini vilabu
vinne vinavyocheza kwenye ligi mbalimbali za soka ulimwenguni.
Twente, Santos, Sint Truiden na Sevilla zilitozwa faini na
FIFA kwa madai ya kuhusisha wadhamini wa nje katika suala la uhamisho wa
wachezaji kinyume cha sheria.
Kulingana na maelezo ya FIFA, Twente ya Uholanzi ilitozwa
faini ya Franc 185 000, Santos ya Brazil Franc 75 000, Sint Truiden ya Ubelgiji
Franc 60 000 na Sevilla ya Uhispania Franc 55 000.
Wakati huo huo, Twente, Santos na Sevilla pia zilituhumiwa
kwa ukosefu wa maelezo ya kutosha katika mfumo wa uhamisho wa wachezaji wa
ITMS.
No comments:
Post a Comment