Kwa kua mashabiki wengi sanawa soka duniani walidhani kuwa eti pengine dirisha la usajili
limepigwa kufuli lakini kumbe ni tofauti na fikra zao.
Leo hii pasi na wasiwasi wowote timu ya “Sunderand” imefanya usajili wa kujiongezea
nguvu katika timu yake baada ya kuandikishiana
kataba mlinzi wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue kwa usajili wa muda mfupi
hadi mwisho wa msimu.
Bila ya shaka haya ni mafanikio makubwa kwa timu hii kwakua
sasa itakua na mlinzi mahiri mwenye kuhimili mikikimikiki na mwenye kupendeza
sana machoni mwa watu.
Huyu ni mchezajii wa zamani wa timu ya taifa ya Ivory Coast kipi kilichomfanya
pendeze na kusajili timu hiyo?
Nikutokana na mazoezi aliyokua akifanya pamoja na timu
hiyo,muda mwingi aliutumia akiwa pamoja nao mpaka kumvutia Sam Allardyce, ambaye ameamua
kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 hivi sasa.
Eboue zamani alikipiga
katika timu ya The Gunners lakini baadae
alikuwa hana timu tangu alipoachana na klabu ya Galatasaray
mwishoni mwa msimu uliopita, mchezo wake wa mashindano alicheza siku 672
zilizopita.
Alifanikikiwa kuichezea club ya Arsenal na mwaka 2011 aliondoka katika timu
hiyo na kujiunga na club ya soka ya Galatasaray
huko Uturuki, ambako aliwahi kuibuka mshindi na kupata mataji matatu ya ligi ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment