
Timu ya Mtende leo jioni itashuka dimbani kuvaana na Mabaharia wa KMKM, wakiwa katika hali isiyo ya kuridhisha kwa mashabiki wake katika michezo yake ya ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja msimu huu.
Mtende wamekuwa na historia mbaya katika ligi kuu msimu huu kwani wameshapoteza michezo kumi na moja (11) katika mechi kumi na sita (16) walizocheza, wameshinda michezo miwili (2) tu na wamekwenda sare michezo mitatu (3).

Mtende wanahitaji kupata ushindi mechi zote zilizobaki ili waweze kuwaridhisha mashabiki wake na pia wao wenyewe kujiweka katika mazingira mazuri ya kutoshuka daraja katika ligi kuu.
Kwa upande wa KMKM wao watashuka dimbani wakiwa wameshacheza mechi kumi na sita (16) na wana alaama (24), wakishika nafasi ya sita (6), huku wakiwa wamepoteza michezo minne (4), sare michezo sita (6), na wameshinda mechi sita (6).
No comments:
Post a Comment