Timu ya El-hilal leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 walipo
wafunga Gulioni katika mchezo wa ligi daraja pili wilaya ya mjini uliosukumwa
ndani ya dimba la Amani hapa visiwani Zanzibar.
Mchezo huo uliochezwa majira ya saa nane za mchana, timu ya
El-hilal walikuwa ndio wa mwanzo kuliona lango la wenzao baada ya mchezaji wake
Ussi Ali, lakini Gulioni wakafanikiwa kusawazisha kupitia mchezaji Abdul-Aziz
Janu.
Timu hizo zilicheza mpira wa kuvutia na pia zilikosa nafasi
nyingi za kufunga, lakini mchezaji wa El-hilal Ali Said, ndipo aliposawazisha
makosa yaliyojitokeza kwa wachezaji wenzake baada ya kuupiga mpira kwa kichwa
na kuingia nyavuni moja kwa moja, na kuyafanya matokeo kuwa mabao 2 kwa 1.
Kocha wa timu ya
Gulioni Fahmi Dego amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri
“mchezo ulikuwa ni mzuri,lakini kama kuna hujuma
tunayofanyiwa timu
ya Gulionibasi hujuma hizo zitafeli,kuna watu wanaihujumu hii
timu lakini inshaallah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hii timu itakwenda vizuri
tu, na hizo hujuma zao zitakwisha”. Alisema kocha Dego.
Aidha aliendelea kwa kusema “wapenzi wangu na mashabiki
watulizane, leo tumefungwa tunajipanga zaidi”.
Kwa upande wake Nahodha wa timu ya El-hilal, Ismail Salum
amesema kwamba mchezo ulikuwa ni mzuri lakini hakuacha kutoa malalamiko juu ya
waamuzi
“mchezo ulikuwa ni mzuri japo kuwa marifa hawapo
makini,na viongozi wa mpira
wanawaona,wahusika hawapo makini, lakini wangekuwa wapo makini na wanalifatilia
hili jambo basi lingekuwa tayari
washalitatua”. Alisema Ismail.
Timu ya El-hilal ikiwa imeavalia jezi rangi nyekundu, na
Gulioni wamevaa jezi rangi nyeupe kwa blue bahar.
No comments:
Post a Comment