Katika
mchezo wa ligi daraja la pili wilaya Mjini uliosukumwa jana ndani ya dimba la
Amani mjini Zanzibar Leeds United wamekubali kichapo cha mabao 3-1walipofungwa
na Shangani.
Mabao ya
Shangani yamefungwa na Ali Khamis katika
dakika ya 20 na dakika 47 na bao jengine limewekwa kimyani na Salum Omar mnamo
dakika ya 24.
Lakini kwa
upande wa Leeds United bao la kufutia machozi limefungwa na Omar Rashid katika
dakika 15.
Nahodha wa
timu ya Leeds United Muhamad Issa amesema kuwa tatizo kubwa la kufungwa ni
kutokana na kuchoka sana kutokana na kutokuwepo kwa mazoezi ya pamoja,pia
amesema jua kali ndio tatizo jengine lilopelekea kupoteza mchezo huo.
“tumefungwa
kwa sababu ya kuchoka na wao sio wazuri, timu yetu haina mazoezi ya pamoja kwa
hiyo kila mmoja anacheza kwa uwezo wake binafsi,ushirikiano ni mdogo tunacheza
mechi jua kali na pia mazoezi ya pamoja hatuna”. Alisema Muhamad Issa.
Aidha kocha wa timu ya Shangani Suleiman Hamid amesema kuwa, mchezo
ulikuwa ni mzuri kwani wanacheza kutokana na mazingira ya jua kali katika
sehemu wanazofanyia mazoezi,
“mchezo
ulikuwa hali nzuri tu kwa sababu sisi tulikuwa tunacheza kwa mujibu ya
mazingira ya hali ya hewa iliyokuwepo na uwezo wetu, kwa sababu tulikuwa
tunajitahid kumiliki mpira ili kuweza kutokana na hali halisi kutokana na
wakati mbaya wa jua kali, kwa hiyo tumecheza vizuri na mechi ilikuwa nzuri”
Alisema kocha Suleiman Ole.
Aliendelea kwa kusema,“Kwa kweli
tulikuwa tunafanya mazoezi kwa sababu sisi tuna malengo ya kuingia katika hatua
ya nane bora kwa hiyo ili kuweza kuingia ni kuhakikisha kwamba mechi hii
tunashinda ili kuishinda ni kufanya mazoezi, kutokana na hali ya mazingira sisi
tunafanya mazoezi saa nane lakini pia tunacheza kwa hali halisi ya kiwanja
nacho kinaunguza, kwa hiyo tumecheza na wachezaji wamepokea maagizo ambayo
wamepewa”.Alisema kocha Suleiman .
Katika
mtanage huo kikosi cha Shangani wamevaa jezi rangi ya blue, huku Leeds United
wakiwa wamevaa jezi nyeupe.
No comments:
Post a Comment